Job Ndugai Atoa ONYO Kwa Halima Mdee na Ester Bulaya......
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai leo bungeni amewapa onyo wabunge Halima Mdee pamoja na Easter Bulaya akisema kuwa wanapaswa kutambua kuwa Bunge bado linauwezo wa kuwaita na kuwahoji na kuwapa adhabu kali zaidi ya hiyo walionayo sasa.
Job Ndugai amesema kuwa ameamua kutoa onyo hilo kufuatia wabunge hao kufanya malumbano na bunge huku wengine wakitumia maneno ambayo si mazuri hivyo amewashauri kuwa wamewavumilia kwa mengi lakini kama bado huko waliko wanaendelea na tabia hizo wanaweza kuwaita na kuwapa adhabu kali zaidi ya hiyo waliyonayo sasa.
"Wako wenzetu ambao bunge hili liliwachukulia hatua za kinidhamu mbalimbali baadhi yao wamekuwa wakijaribu kufanya malumbano na bunge na baadhi ya kauli zao zimekuwa ni kauli ambazo si nzuri kihivyo, ningependa kuendelea kuwashauri kwamba tumewavulimilia kwa mambo mengi lakini kama bado huko waliko wanafikiri wanaweza kuendelea na tabia hizo huko waliko wajue kabisa bado tunaweza kuwaita, tukawajadili kwenye bunge hili na kuwachukulia hatua kali zaidi ya hii waliyonayo, kama mtu anataka kwenda mahakamani unaalika watu kama mkutano wa hadhara si unaenda tu" alisisitiza Job Ndugaina kuongeza;
"Mimi nawapa onyo tu la jumla kama ni viongozi ni vizuri kuongea lakini ongea vitu ambavyo unataka kuongea lakini ukitaka kupambana na watu wengine nao watataka kupambana na wewe, kwa hiyo mtapimana"alisema Job Ndugai
Spika wa Bunge, Job Ndugai ametoa kauli hii siku moja baada ya kusifiwa na Rais John Pombe Magufuli kuwa anakwenda vizuri kuwadhibiti watu ambao wanaropoka bungeni na kumwambia kuwa aendelee na moto huo huo ili watu hao wakiropoka nje ya bunge adili nao.
Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliwaadhibu wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya kutohudhuria vikao vyote vya Bunge linaloendelea hadi Bunge la Bajeti 2018/2019 baada ya kuwakuta na hatia ya kudharau mamlaka ya Spika wa Bunge.

Post a Comment