Lindelof kuondoa madhaifu ya Man u
Klabu ya Manchester United ipo katika mkakati wa kujitengeneza ili kurudisha heshima na kati ya maeneo ambayo kocha wao Jose Mourinho anapambana kuyaimarisha ni eneo la ushambuliaji pamoja na eneo la ulinzi ambalo limekuwa haliaminiki.
Katika eneo la ulinzi Mourinho kwa muda sasa amekuwa akihusuishwa na kutaka kumsajili mlinzi wa klabu ya Benfica na timu ya taifa ya Sweden Victor Lindelof ili kutengeneza ukuta mgumu katika timu hiyo inayojiandaa na Champions League msimu ujao.
Taarifa rasmi kutoka katika klabu ya Manchester United imethibitisha kwamba klabu hiyo imeshafikia makubaliano na Lindelof na sasa kinachosubiriwa ni kwa mlinzi huyo kusafiri hadi katika jiji la Manchester wiki ijayo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya.
Lindelof mwenye miaka 22 ameitumikia timu ya taifa ya Sweden michezo 12 huku akiitumikia Benfica katika michezo 47 na sas euro 32m zinamtoa Benfica na kwenda kujiunga na Manchester United.
Post a Comment