Samatta sababu za kiufundi Taifa stars kutoa sare..
Matokeo ya sare ya kufungana 1-1 kati ya Taifa Stars dhidi ya Lesotho, hayakuwa mabaya kwa mashabiki pekee, bali hata kwa wachezaji na benchi lao la ufundi lakini nahodha wa Stars Mbwana Samatta yeye alishindwa kuzuia hasira zake na kuonesha wazi kuwa alikasirishwa na matokeo hayo.
Samatta amekiri mbele ya waandishi wa habari kuwa, licha ya kutopenda kushindwa lakini hajafurahishwa na matokeo ya kufungana 1-1 na Lesotho huku Stars ikiwa nyumbani mbele ya mashabiki wake kibao.
“Mimi sipendagi kushindwa, hata draw sijaifurahia kwa sababu tulikuwa tunacheza nyumbani na ukizingatia ni hatua ya makundi tulikuwa tunahitaji ushindi kwa lazima kwa hiyo tumepata draw sio mbaya lakini haikuwa katika akili yangu kwamba tupate draw dhidi ya Lesotho nyumbani wakati tulikuwa tunahitaji ushindi ili kujitengenezea mazingira mazuri kwenye kundi.”
“Nafikiri wachezaji wote walikuwa na hasira sio mimi pekeyangu labda nilishindwa kujizuia kutoionesha lakini hakuna mtu ambaye amefurahia matokeo haya.”
Lakini Sagoal amesema hata uwanja wa Azam Complex umechangia Stars kushindwa kufanya vizuri kwa sababu ni mdogo na ulikuwa unawanyima wachezaji nafasi hasa muda ambao Lesotho waliamua kutumia mbinu ya kujilinda zaidi huku Stars wakitaka kushambulia.
“Ukiangalia uwanja wa taifa na Azam Complex kuna tofauti, ukicheza kwenye uwanja wa taifa kuna kuwa na nafasi zinaonekana lakini hapa (Azam Complex) kitu ambacho kimewasaidia Lesotho ni uwanja kuwa mdogo kwa sababu waliweza kukaa nyuma na mipira yote ambayo ilikuwa inapokelewa na wachezaji wetu mmchezaji wao mmoja au wawili walikuwepo. Kwa hiyo mimi nafikiri uwanja umewasaidia.”
Post a Comment