Mpinzani wa Malinzi ajitokeza...
Wakati uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ukitarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu mkoani Dodoma, hatimaye nafasi ya urais wa shirikisho hilo imepata wapinzani wawili hadi sasa.
Jamal Malinzi ambaye ni rais wa sasa wa shirikisho hilo amechukua fomu ya kutetea nafasi yake lakini amepata mpinzani.
Muda mfupi baada ya Malinzi kuchukua fomu ya kutetea nafasi yake hiyo, ndipo mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Yanga, Iman Madega naye akatinga maguu kwenye ofisi za shirikisho hilo kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuwania urais wa TFF.
Madega amechukua fomu hiyo leo asubuhi katika ofisi za shirikisho zilizopo Karume jijini Dar es Salaam, hiyo ni dalili njema kwa wanamichezo ambapo awali ilionekana kama Malinzi hatakuwa na mpinzani katika nafasi yake.
Malinzi ndiye anayeshikilia kiti hicho kwa takribani miaka minne iliyopita.
Amekuwa akishutumiwa kushindwa kusaidia kupatikana kwa mabadiliko.
Hata hivyo, yeye amekuwa akisisitiza kwamba amefanya mengi.
Leo amechukua fomu kuthibitisha kuwa atawania miaka minne ijayo.
Post a Comment