Manchester United Wanaswa wakimfukuzia Fabinho Tavares
WAKALA wa Jose Mourinho, Jorge Mendes, ameonekana akipata chakula cha jioni na mteja wake Fabinho Tavares (pichani), anayetajwa kufukuziwa na Manchester United, lakini mazungumzo yao yaliegemea uhamisho wa nyota huyo kwenda Atletico Madrid.
Fabinho anayemudu nafasi ya beki na kiungo ni mmoja wa wachezaji wanne waliobaki katika orodha ya wanaofukuziwa na Mourinho baada ya kocha huyo kukamilisha usajili wa beki wa kati wa Benfica, Victor Lindelof
. Wengine ni straika wa Real Madrid, Alvaro Morata, winga wa Inter Milan, Ivan Perisic na straika wa Torino, Andrea Belotti
. Kwa mujibu wa gazeti la AS, Mendes na Fabinho walikutana na Mtendaji Mkuu wa Atletico Madrid, Miguel Angel Gil Martin katika hoteli moja maarufu katikati ya jiji la Madrid Jumanne usiku, hivyo kuibua tetesi mpya kuwa anaweza kumkacha Mourinho na kwenda kufanya kazi na Diego Simeone.
Kama nyota huyo atachagua kwenda Atletico, atalazimika kusubiri hadi Januari mwakani aweze kucheza kutokana na klabu hiyo kutumikia adhabu ya Fifa ya kutosajili wachezaji wapya hadi mwakani baada ya kusajili wachezaji chini ya miaka 18.
Post a Comment