Mugabe amfuta kazi mkuu wa mashtaka Zimbabwe



Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amemfuta kazi mkuu wa mashtaka wa nchi hiyo Jonannes Toanana, baada ya jopo la uchunguzi kumpata na hatia ya ukosefu wa nidhamu na uzembe.

Bwa Tomana ambaye wakati mmoja alikuwa mshirika mkubwa wa Rais, alisimamishwa kazi mwezi Februari mwaka uliopita.

Aliondolewa ofisini baada ya kutupilia mbali mashtaka dhidi ya wanaume wawili waliodaiwa kupanga njama ya kulipua kiwanda cha maziwa kinachomilikiwa na mke wa Rais Mugabe.

Vyombo vya habari saa vinasema kuwa Tomana sasa atajibu mastaka kwenye mahakama ya juu kwa makosa ya matumizi mabaya ya mamlaka.

No comments

Powered by Blogger.