Wafungwa watoroka kutoka kituo cha polisi DRC
Watu wenye silaha wameshambulia ofisi ya mkuu wa mashtaka na kituo cha polisi kwenye mji mkuu wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Kinshasa na kusababisha wafungwa kadha kutoroka.
Kuna ripoti tofauti kuhusu ni wafungwa wangapi walifanikiwa kutoroka.
Redio inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa ya Radio Okapi, inasema kuwa wafungwa 17 walitoroka, wengi kutoka kwa kituo cha polisi.
Mtandao mmoja wa habari nchini Congo wa Politico, unasema kuwa washambuliajia walikuwa ni wanachama wa Bunda dia Kongo ambalo ni kundi la dini lililo na mtazamo wa siasa.
Serikali inalilaumu kundi hilo kufuatia shambulizi lililotokea katika gereza kuu la Kinshasa mwezi uliopita ambapo mamia au hata maelfu ya wafungwa walitoroka.
Post a Comment