Simba na Yanga kigugumizi kwa Boukungu









BEKI mkongwe Janvier Besala Boukungu ni sawa na “home work” kwa Kamati ya Usajili na ile ya ufundi ya Simba. Kwamba abaki au aende, hakuna ambae ana uhakika wa asilimia kwa kuwa kuna mambo yanachanganya.

 Imeelezwa kati ya wajumbe, wapo wanaoona wakati umefika aende na wengine wanaona angalau msimu mmoja aongezewe. “Unajua kweli umri wa Boukungu umekwenda, lakini alionyesha weledi sana


. Uwanjani alijituma na nje ya uwanja alikuwa ni professional kabisa,” kilieleza chanzo. Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe yeye alisema kazi ya Boukungu ilikuwa bora na wanaona atabaki lakini kuna viongozi wanaamini ni vyema wakamruhusu kwa heshima na wakampongeza kwa kazi yake nzuri ili aondoke.

No comments

Powered by Blogger.