Wilshare majeraha yambakiza Arsenal...
KLABU ya Arsenal inajipanga kumwacha kiungo wao Jack Wilshere nchini England ambako ataendelea kuuguza maumivu yake ya mguu uliovunjika, hali itakayomkosesha nafasi ya kuichezea timu yake kwenye pre-season Australia na China
. Kiungo huyo alipata jeraha hilo msimu uliopita na kujikuta akikosa wiki za mwisho za kuibeba timu aliyokuwa akiiochezea kwa mkopo ya Bournemouth.
Wilshere atafanyiwa scan siku chache zijazo ili kuchunguza maendeleo ya jeraha lake kabla ya kuruhusiwa kuanza mazoezi ya taratibu.
Kama kila kitu kitaenda vizuri, kiungo huyo ataanza mazoezi na klabu yake pindi atakaporudi London.
Post a Comment