SAFARI YA ANTONIO CONTE' KUINOA CHELSEA YAINGIA VIKWAZO..FITINA ZA CHINI CHINI ZAANZA KUMTAFUNA..



Pamoja na ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Tottenham Hotspur mwishoni mwa wiki lakini taarifa zinadai Chelsea wako katika mpango wa kumfukuza kocha Antonio Conte.

Antonio Conte amekuwa na majanga mengi tangu baada ya ligi kuisha na kuipa Chelsea ubingwa na inasemekana hayuko katika wakati mzuri na watu wengi klabuni hapo.

Antonio Conte amekuwa na madai mengi ndani ya klabu ya Chelsea kuhusu masuala ya usajili na mambo mengine mengi ikiwemo masuala ya academy ya soka ya Chelsea.

Conte amekuwa chanzo cha Chelsea kutokuwa sawa na mfungaji wake mahiri Diego Costa na matatizo haya yote yanamuweka Conte njia panda kuendelea kufundisha darajani.

Mkurugenzi wa Chelsea Marina Granovskala inasemekana tayari ameanza kufikiria kumtosa Conte na pia ameshapata mtu atakayechukua nafasi ya Muitaliano huyo.

Thomas Tuchel wa Borussia Dortmund ndiye mtu anayetajwa kuchukua nafasi ya Conte na tayari Chelsea wanajipanga kuanza mazungumzo na kocha huyo.

Gazeti maarufu la michezo nchini Ujerumani la Bild limesema uhusiano wa Conte na mkurugenzi wake Marina sio mzuri kwa sasa na hii inamfanya Marina atafute mtu sahihi.

Antonio Conte alijiunga na Chelsea katika msimu uliopita wa ligi na katika msimu wake wa kwanza tu aliwamba kombe la ligi ya Epl lakini sasa hali inaonekana kubadilika.

No comments

Powered by Blogger.