SIMBA YAZIHIRISHA USAJILI WAKE..
Simba inesginda Ngao ya Jamii kwa kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya timu zote kutofungana ndani ya dakika 90.
Hii ni Ngao ya Jamii ya tatu kwa Simba katika historia tangu kuanzishwa kwa ngao hiyo mwaka 2001.
Simba walitwaa kwa mara ya kwanza mwaka 2011 kwa kuifunga Yanga 2-0, mwaka 2012 wakabeba tena mbele ya Azam kwa ushindi wa magoli 3-2 kisha mwaka huu wameifunga Yanga kwa penati 5-4.
Yanga ndio timu pekee ambayo imechukua Ngao ya Jamii mara nyingi zaidi tangu ilipoanzishwa. Yanga imeshinda mara tano (2001, 2009, 2010, 2013 na 2014).
Azam na Mtibwa Sugar wamefanikiwa kuchukua Ngao ya Jamii mara mara moja.
Post a Comment