CCM YATOA TAMKO BAADA YA TUKIO LA TUNDU LISSU KUSHAMBILIWA NA RISASI.....
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole kimelaani kitendo alichofanyiwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kwa kupigwa risasi leo mchana nyumbani kwake Dodoma.
Taarifa hiyo ya CCM inalaani kitendo hicho cha kikatili na kusema si kitendo cha utu hivyo kimelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa tukio hilo na kuwachukulia sheria kali wote ambao watapatikana kuhusika katika tukio hilo.
Post a Comment