RAPA NA MUIMBAJI WA ZAMANI WA TWANGA PEPETA MSAFIRI DIOF AREJEA BONGO KWA MAPUMZIKO...

Image result for picha za msafiri diouf

Rapa na mwimbaji wa zamani wa Twanga Pepeta Msafiri Diouf ambaye kwasasa anafanya muziki London, Uingereza, amerejea Bongo kwa mapumziko mafupi.

 Diouf ameiambiaKabasele news kuwa aliingia Dar es Salaam juzi usiku na anatarajiwa kuwa hapa nchini kwa muda usiopungua mwezi mmoja. “Mwaka jana nilikuja na kukaa kwa wiki tatu, safari hii natarajia kukaa angalau kwa mwezi mmoja na wiki moja au mbili,” alisema Diouf.

 Mwanamuziki huyo anasema hajaja mikono mitupu bali atakuwa na zawadi ya nyimbo tatu mpya atakazozirekodi hapa Dar es Salaam ndani ya siku chache zijazo.

 Wiki ijayo Diouf ataingia studio za C9 Records kufyatua wimbo wa kwanza uliopewa jina la “The Bridge”.kabasele news ilikuwepo C9 Records wakati Diouf akifanya ‘booking’ ya kurekodi ngoma hiyo ya “The Bridge” ambayo amesema itakuwa na vionjo vya reggae.

No comments

Powered by Blogger.