HALI YA KIPA WA MANCHESTER CITY YAIMARIKA ARUDI UWANJANI KWA KASI ZAIDI....



Kipa wa Manchester City, Ederson amerejea kwenye mazoezi lakini ameonyesha jinsi ambavyo alivyoumia usoni katika purukushani za kuwania mpira kati yake na mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane.

Kipa huyo mwenye miaka 24 alitolewa uwanjani akiwa katika machela maalum baada ya kuumia usoni katika mchezo huo wa Jumamosi iliyopita.

Huu ni msimu wake wa kwanza akiwa City tangu aliposajiliwa kwa pauni milioni 35 akitokea Benfica ya Ureno.

Katika mazoezi ya jana alionekana akiwa amevaa kifaa maalum kuziba uso wake kwa pembeni ambapo alishonwa nyuzi kadhaa kutokana na kuchanika.

No comments

Powered by Blogger.