''AJIBU ANA KIWANGO CHA JUU SANA SIO YULE ALIEKUA SIMBA HIVYO SIMBA KUWENI MAKINI''JULIO..
Kocha
wa Dodoma FC ya Mkoani Dodoma, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameitaka timu
yake ya zamani ya Simba kuwa makini na mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim
Ajibu, Jumamosi katika mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga.
Jumamosi
kuna mchezo wa Simba na Yanga na mashabiki wamekuwa wakiusubiri kwa
hamu kubwa kuona ni timu gani inaweza kuibuka na ushindi.
Julio
ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba na kocha wa timu hiyo amesema
kuwa Simba wanatakiwa kumlinda sana mshambuliaji huyo kwa kuwa sasa
amebadilika siyo kama zamani.
Julio
alisema, mchezo huo unatarajia kuwa mgumu na wenye upinzani wa hali ya
juu na kuwataka Simba wasiibeze Yanga kwa kuwa ina kikosi kizuri na
wanacheza mpira wa kueleweka.
“Ajibu
ni mchezaji mzuri ana kiwango cha hali ya juu sio yule aliyekuwa Simba,
hivyo ni mchezaji wa kuchungwa sana katika mchezo huo, naamini mchezo
huo utakuwa mgumu na wenye upinzani wa hali ya juu.
“Simba
wanahitaji kuwa makini na siyo kama nasema vibaya ila naamini kutakuwa
na ushindani mkubwa katika mechi hiyo ijapokuwa naamini mechi itakuwa na
ugumu wa hali ya juu kutokana na kila upande kujiandaa ipasavyo.
“Mechi
hii mara nyingi huwa inakuwa haina mwenyewe kutokana na kila upande
kujiandaa vyema kuelekea mchezo huu hivyo tunasubiria siku ya Jumamosi,”
alisema Julio.
Post a Comment