''NIPO FITI KUKABILIANA NA SIMBA NA HUYO OKWI WANAEMSIFIA YUPO VIZURI'' KELVIN YONDANI.......
Wakati joto la mechi ya watani linazidi kupanda, beki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani, amesema kuwa, Jumamosi ijayo atahakikisha anamzuia ipasavyo straika wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi na watu watamsahau.
Jumamosi ijayo, Yanga itapambana na
Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa katika Uwanja wa Uhuru
jijini Dar ambapo mchezo huo unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki
wengi wa soka wa ndani na nje ya Tanzania.
Okwi ambaye kwa sasa anaongoza kwenye
chati ya wafungaji katika Ligi Kuu Bara akiwa na mabao nane, anatarajiwa
kufanya makubwa kwenye mchezo huo ikiwemo kuisumbua vilivyo ngome ya
ulinzi ya Yanga.
Kutokana na hali hiyo, Yondani amesema:
“Katika mchezo wetu uliopita dhidi ya Stand United sikucheza kwa sababu
makocha walikuwa wakihofia pengine ningepewa kadi ya njano ambayo
ingesababisha niikose mechi dhidi ya Yanga na wala sikuwa majeruhi.
“Hivyo nipo fiti kukabiliana na Simba na
huyo Okwi ambaye wanamsifia kwamba yupo vizuri, nitamkaba na
watamsahau,” alisema Yondani ambaye amewahi kucheza na Okwi Yanga.
"Hata hivyo, Okwi anakwenda kwenye
mchezo huu akiwa na heshima ya kuwafunga Yanga mabao matatu kwa kipindi
chote na mechi hizo zote Yondani alikuwa uwanjani.
Post a Comment