ZITTO KABWE AACHIWA KWA DHAMANA..
KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameachiwa kwa dhamana leo Jumanne jioni baada ya kushikiliwa na polisi akihojiwa jijini Dar es Salaam.
Zitto baada ya kuhojiwa katika Kituo cha Polisi cha Chang’ombe mkoani Temeke sasa alihamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu amesema baada ya Zitto kuhojiwa kuhusu aliyozungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za udiwani zilizofanyika Kijichi Jumapili Oktoba 29,2017 aliachiwa kwa dhamana.
Shaibu amesema Zitto aliyewakilishwa na wanasheria Venance Msebo na Steven Mwakibolwa alidhaminiwa na watu wawili na alitakiwa kurudi kituoni hapo Jumatatu Novemba 6,2017. Hata hivyo, amesema alikamatwa tena
Post a Comment