Diamond Adai Hana Uwezo wa Kumlipa Hamisa Mobeto Milioni 5 kwa Mwezi za Matunzo ya Mtoto
Msanii
Nasib Abdul maarufu Diamond Platinumz, amedai mahakamani kuwa hana
uwezo wa kumlipa Mwanamitindo Hamisa Mobeto, Sh milioni tano kama
gharama za matunzo ya mtoto kwa mwezi.
Diamond
amewasilisha majibu hayo katika Mahakama ya Watoto Kisutu, mbele ya
Hakimu Mkazi Devotha Kisoka baada ya Mobeto kumfungulia kesi ya madai
katika Mahakama hiyo ya watoto akidai mambo mbalimbali ikiwamo matunzo
ya mtoto.
Katika
majibu yake Diamond amedai fedha hizo anazodai Hamisa kulipwa kwa mwezi
kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.
Mobeto
katika maombi yake kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter
Godluck wa Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys, anaiomba mahakama
imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto kila mwezi, mtoto huyo wa kiume
aliyezaa na msanii huyo na kumuomba msamaha kwa umma kwa kumsababishia
madhara yaliyoishtua familia yake.
Baada
ya kupokea majibu hayo mahakama iliahirisha kesi hiyo ya madai hadi
Novemba 8, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Mobeto kupitia wakili wake
walimpa notisi Diamond ya kutaka amwombe radhi na kupeleka matunzo ya
mtoto ndani ya siku saba lakini notisi hiyo haikutekelezeka hivyo
aliamua kulifikisha suala hilo mahakamani.
Post a Comment