MADRID DERBY NDANI YA UEFA CHAMPIONS LEAGE VITA NYINGINE YA ZIDANE NA SIMEONE
Usiku wa leo moto unawaka pale Santiago Bernabeu ambapo Real Madrid watawakaribisha Atletico Madrid katika nusu fainali ya kwanza ya ya michuano ya UEFA.
Kuelekea mchezo huo, karibia makocha kutoka kila pande wamekuwa hawajiamini kuhusiana na derby huyo kwani kila mmoja maongezi yake anaonekana kumhofia mwenzake, suala linaloufanya mchezo huu kuonekana mgumu.
Zinedine Zidane kwa upande wake amekataa kabisa kauli za wanaosema Real ndio wana nafasi kubwa kuifunga Atletico na kocha huyo amesisitiza wanahitaji umakini wa ziada.
“Huwezi kutupa nafasi sisi wakati hii ni hatua ya mtoano, hapa ni 50-50, ugumu na upinzani wa Atletico haujawahi kubadilika toka nikiwa mchezaji na leo tunapaswa kufanya kila namna ili kushinda” alisema Zidane.
Zidane ameongeza kuwa kila mwaka Atletico wanakuwa bora kuliko msimu uliopita, na mara zote wanapambana sana na hawajawahi legeza lakini akasisitiza kwamba kuingia nusu fainali ina maana wao pia ni bora.
Kwa upande wa kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone yeye amesema leo wataungana kuanzia mioyo ili kuunganisha nguvu za wana Atletico kwenda kuikabili Real Madrid.
“Naona kabisa mchezo mgumu sana na wapinzani wetu watajaribu kutumaliza dakika za mwanzo jambo tunalopaswa kuwa makini nalo, inabidi mchezo huu tuucheze kwa jinsi tunavyofurahia” alisema Simeone.
Atletico wanaenda katika mchezo huu na tatizo kubwa la mlinzi wa kulia kwani Jose Gimenez na Juanfran watakosa mchezo huo huku Sime Vrsaljko nae akiukosa mchezo huo
Post a Comment