MBWANA SAMATTA AWADATISHA MASHABIKI WA KRC GENK...
Ukisema mambo yanaanza kunyooka, baada ya mashabiki wengi wa KRC Genk kuonyesha imani kubwa kwa mshambulizi, Mbwana Samatta.
Samatta anaonekana kuwa bora zaidi kutokana na kuwa tegemeo katika kikosi cha Genk cha Ubelgiji.
Imeonekana mmoja wa shabiki akiwa na bango uwanjani, akiomba jezi ya Samatta.
Imekuwa kawaida kwa mashabiki wa Ulaya kuomba jezi kwa wachezaji wanaowapenda wakitumia mabango kama shabiki huyo wa Genk.
Samatta amekuwa akifunga mfululizo na wakati mwingine kushindwa kufanya hivyo kwa kipindi fulani lakini imani kwa benchi la ufundi na mashabiki inaonekana kupanda kwa kiwango cha juu kabisa.
Post a Comment