MYAMA ANAZIDI KUUNGURUMA KWA AFRICANS LYON


Dakika ya 34: Omary Salum wa African Lyon anapata kadi ya njano kwa kumchezea faulo Kichuya.

Dakika ya 30: Beki wa Simba, Boukungu anapanda mara kadhaa mbele kusaidia kutengeneza mashambulizi.

Dakika ya 28: Kichuya anawatoka walinzi wa Lyona na kupiga shuti kali lakini linatoka nje la lango.

Dakika ya 24: Simba wanaendelea kutawala mchezo.

Dakika ya 18: Lyon wanafika langoni mwa Simba na kupata kona mara mbili mfululizo lakini wanashindwa kuzitumia vizuri.

Dakika ya 15: Simba wanalishambulia lango la Lyona lakini Ajibu anashindwa kutumia nafasi anayopata baada ya kutengenezewa nafasi na Kichuya.

Dakika ya 13: Simba wameanza kutawala mchezo, wanaumiliki muda mwingi, jua nalo limeanza kutoka kwa kuwa mvua imekuwa ikinyesha kwa wingi jijini Dar.

Dakika ya 10: mchezo bado haujawa na kasi, timu zote ni kama zinasomana.

Dakika ya 5: Simba nao wanajibu mapigo kwa kushambulia kupitia kwa Laudit Mavugo.

Dakika ya 3: African Lyon wanafanya shambulizi kwenye lango la Simba.

Dakika ya kwanza mchezo umeanza.

Kikosi cha simba kinachoanza dhidi ya African Lyon hii leo
1. Daniel Agyei


2. Besala Boukungu
3. Mohamed Zimbwe 
4. James Kotei
5. Juuko Murshid
6. Jonas Mkude (Nahodha)
7. Shiza Kichuya
8. Mzamiru Yassin
9. Laudit Mavugo
10. Ibrahim Ajibu
11. Mohamed ibrahim

AKIBA
Manyika
Vincent
Novat
Kazimoto
Liuzio
Blagnon

Pastori

No comments

Powered by Blogger.