SINTOFAHAMU KWA WANACHAMA NA MASHABIKI WA YANGA BAADA YA TAARIFA YA KUJIUZULU YUSUF MANJI.....
WANACHAMA na wapenzi wa Yanga wamepatwa na mishtuko mkubwa baada ya taarifa kuzagaa kwamba mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji amejiuzulu nafasi yake hiyo. Mei 23, mwaka huu kulikuwa na barua iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha kuwa Manji ameachia uenyekiti wa klabu ya Yanga na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clementi Sanga atakaimu
Wanachama na wapenzi hao kwa nyakati tofauti walitoa maoni yao kuhusu kujiuzulu kwa Manji huku wengi wakitaka aendelee kuisaidia timu hiyo hasa katika kipindi hiki cha usajili. Mwanachama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Ally Hassan kutoka jijini Dar es Salaam alisema kwamba hana tatizo na uamuzi wa Manji lakini anachomuomba mwenyekiti huyo ni kuendelea kuisaidia klabu hiyo kwenye usajili.
“Mimi namuomba Manji aendelee kuisaidia timu yetu hata kama ameamua kujiweka pembeni sababu kipindi hiki cha usajili ni kigumu sana kwetu hivyo aendelee kusaidia timu kwenye usajili.”
Mwanachama mwingine aliyejitambulisha kwa jina la John Haule kutoka Mbagala jijini Dar es Salaam alisema Kwamba ameshitushwa mno na taarifa hizo lakini anachoomba ni kwa Manji kuendelea kuisaidia timu hiyo katika usajili.
“Unajua tuna wachezaji wa kigeni ambao wanalipwa mishahara mikubwa sana, hatutaweza kuendelea kuwalipa wachezaji hawa hivyo namuomba Manji aendelee kuisaidia timu yetu. Mashabiki walikuwa ni wengi waliozungumza na mtandao huu ambapo wengine walionekana kushitushwa mno taarifa hivyo na kuwekwa kwenye hali ya sintofahamu.
Post a Comment