Manchester United kurudisha karata yake kwa hyu endapo ikimkosa Morata

Kuna tetesi zinadai Alvaro Morata huenda akajiunga na Manchester United lakini zingine zinadai United watashindwana na Real Madrid litakapokuja suala la kifedha kwani miamba hiyo ya nchini Hispania inataka kiasi kikubwa cha pesa ambacho United wanaona ni zaidi.
Mabosi wa Manchester United wanapambana sana kumtafuta mshambuliaji namba 9 haswa baada ya klabu hiyo kuacha kumuongezea mkataba mpya Zlatan Ibrahimovich ambaye ndiye alikuwa namba 9 wao tegemezi katika msimu ulioisha wa ligi kuu.
Kutokana na ugumu wa kumpata Alvaro Morata mabosi wa United wanaona kama wakishindwa kumpata ni bora waongeze fedha katika hela waliyotaka kumnunulia Morata na kuitumia pesa hiyo kujaribu kumshawishi upya mshambuliaji Antoine Griezman aweze kujiunga nao.
Griezman mwanzo aliwatolea nje Manchester United na kuamua kubaki katika klabu ya Atletico Madrid lakini United wanaonekena hawajakata tamaa na sasa wanarudi tena kwa Antoine Griezman ambaye wanaona ndio mtu sahihi kukaa katika nafasi ya Zlatan Ibrahimovich.

No comments

Powered by Blogger.