Pele aibuka na kumchana Paulo Dyabala.


Siku za karibuni mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Juventus Paulo Dyabala amekuwa gumzo sana kutokana na uwezo wake, Dyabala kuna kipindi alionekana kama tegemezi kubwa la Waargentina wengi wakimuona dogo huyo kuchukua nafasi ya Lioneil Messi.
Paulo Dyabala amekuwa bora sana haswa na timu ya Juventus kiasi cha kuvivutia vilabu vikubwa duniani na wachambuzi wengi wa soka wamekuwa wakisema Paulo Dyabala anafanana kiuchezaji na gwiji wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina Diego Maradona.
Mwanasoka bora anayetajwa kuwahi kutokea duniani ambaye alikuwa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil Pele ameibuka na kumkandia vikali Paulo Dyabala na kusisitiza kwamba Dyabala bado sana kufikia kiwango anachotajwa kuwa nacho.
Pele amesema Dyabala sio lolote “kwanza sio bora kama watu wanavyomzungumzia lakini pia nashangaa wanaomfananisha na Diego Maradona wakati hawafanani hata kidogo na kitu pekee wanachofanana ni kutumia mguu wa kushoto kucheza mpira” alisema Pele.
Katika misimu miwili ya ligi kuu nchini Italia Paulo Dyabala mwenye umri wa miaka 23 ameifungia Juventus jumla ya mabao 30 na akiisaidia kubeba kombe la Serie A lakini alikuwepo uwanjani wakati wa fainali ya Champions League ambapo Juventus walikubali kipigo cha mabao 4 kwa 1 toka kwa Real Madrid.

No comments

Powered by Blogger.